Exodus 36:20-34

20 aWakatengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani. 21Kila mhimili ulikuwa na urefu wa dhiraa kumi,
Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.
na upana wa dhiraa moja na nusu,
Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5.
22zikiwa na ndimi mbili zilizokuwa sambamba kila mmoja na mwingine. Wakatengeneza mihimili yote ya maskani jinsi hii. 23Wakatengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani, 24na wakatengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. 25Kwa upande wa kaskazini wa maskani wakatengeneza mihimili ishirini 26na vitako arobaini vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. 27Wakatengeneza mihimili sita kwa mwisho ulio mbali, yaani upande wa magharibi wa maskani, 28na mihimili miwili ikatengenezwa kwa ajili ya pembe za maskani za upande uliokuwa mbali. 29 dKatika pembe hizi mbili mihimili yake ilikuwa miwili kuanzia chini mpaka juu, na ikaingizwa kwenye pete moja; mihimili ya pembe hizi mbili ilifanana. 30Kwa hiyo kulikuwa na mihimili minane, na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili.

31 eWakatengeneza pia mataruma kwa mti wa mshita: matano kwa ajili ya mihimili ya upande mmoja wa maskani, 32matano kwa ajili ya mihimili ya upande mwingine, na matano kwa ajili mihimili ya upande wa magharibi, mwisho kabisa mwa maskani. 33Wakatengeneza taruma la katikati, likapenya katikati ya mihimili kutoka mwisho mmoja hadi mwisho mwingine. 34Wakaifunika hiyo mihimili kwa dhahabu, na wakatengeneza pete za dhahabu za kushikilia hayo mataruma. Pia wakayafunika hayo mataruma kwa dhahabu.

Copyright information for SwhNEN